Monday, January 4, 2010

MAKTABA ZINAZOUNGUA, VIJANA TUMEZITUMIA KWA KIASI GANI?







Mwaka 2009 umeisha vibaya kwa watanzania wazalendo na wanaojua historia ya nchi hii. Tulimpoteza mmoja wa waasisi muhimu wa nchi hii, Mzee Rashid Mfaume Kawawa. Naona faraja na furaha kwa kuwa mmoja wa vijana wanaojua mchango wa viongozi wetu waliopita. Viongozi ambao wakati wa utawala wao hawakugubukwa na tamaha za mali na wizi(ufisadi).

Nasikitika kwa sababu vijana wenzangu wengi wa sasa hatuwafamu watu hawa wala atujui mchango wao.
Tunachotakiwa kufahamu ni kwamba vifo vya wazee kama Hayati Mwl. Julius Nyerere na Hayati Rashid Mfaume Kawawa ni sawa na maktaba inayoungua. Ushauri wao na uwepo wao unasaidia sana muenendo wa serikali yetu. Ni watu wenye uzoefu na wameona mengi, ushauri wao ulikuwa na umekuwa wa muhimu na wenye mtazamo wa kati, nikimaanisha wakiangalia sio matajiri tu bali na hata maskini.

Tumepoteza watu muhimu sana, lakini hicho si cha kuongelea kwa sana kwa sasa tuangalie je kwa wale ambao bado wapo hai, TUNAWATUMIAJE?

No comments: