Sunday, February 14, 2010

VIJANA WA TZ NA CULTURE!! UTAMADUNI!


SAUTI ZA BUSARA;Mfano wa positive side ya globalization effect- easy culture exchange!


Wazazi na wazee wetu wengi wanalamamika kuhusu tabia zetu vijana wa sasa. Mara hiki mara kile, je, kuna kweli maadili yameshuka? Ni sahihi kusema vijana wa sasa tunauacha utamaduni wa wazazi wetu, na je tunafanya makosa by doing so? Kila mtu anamtazamo wake ila mimi nashusha wangu.

Kwanza, hadi leo sijatambua utamaduni wa asili wa mtanzania. Naamini hakuna utamaduni unaowezwa kuitwa wa asili wa watanzania kwa sababu ndani ya Tanzania tuna zaidi ya makabila 120 nao wote wanatamaduni zilizo'completely different from one another. Kitu pekee tunachoweza kuita identity ya mtanzania ni the swahili language. Anayebisha aseme....

Kila kabila lina utamaduni wake, kwa hiyo nachoamini as vijana wengi wa sasa tunaokulia mbali na mazingira ya kabila zetu{mijini} lazima tukue tofauti na matarajio ya wazazi na wazee wengi.

Tunazungukwa na watu wa tamaduni mbalimbali as we live together and interact tunachagua tabia mbalimbali toka interaction tofauti kama marafiki, tunachoona kwenye television na other sources of media.
Hiki kizazi cha 'globalization', kutokana na hili kuna postive na negative effects. Lakini ninachotaka mkubaliane na mimi ni kwamba wetu wengi wamekuwa waki'base kwenye negative effects bila kuangalia upande mwingine wa shilingi na hiyo ni makosa.
Kwa mfano kuna hii issue ya mavazi; eti mtu akivaa nguo fupi au inayoonesha sehemu kubwa ya mwili ni tatizo siku hizi, watu watasema siyo utamaduni wetu....MIMI NABISHA! Tutumie kisingizio kingine lakini si point ya utamaduni, hii ni kwa sababu utamaduni wa waafrika kalibia wote mavazi yao mengi yalikuwa na bado yanaonesha sehemu kubwa za mwili wao.







WOMEN OF EKITI TRIBE OF NIGERIA.







NDEBELE; Mfano wa Vazi la heshima hasa kwa wanawake walioolewa. Binti wa kibongo akionesha kitovu mzungu atalaumiwa!!





VIJANA WA KIZULU;Sehemu kubwa ya miili yao ipo uncovered.



JE KING MSWATI ANAKOSEA? Ila anafuata utamaduni....!!!
Madada zetu wanavaa lakini kiuhalisia hawajawafikia hawa!

Kwa hiyo kwa mtazamo wangu mabadiliko makubwa ni vitu kama the use of cocaine na prostitution ndo tunaweza kuita mabadiliko mabaya ya kiutamaduni. Mambo ya kusema kuanza mapenzi mapema kwa vijana wa miaka kumi na nane hadi ishirini na kitu sio kitu cha kulaumu utamaduni wa nje na globalization. Tamaduni nyingi kama si zote za Africa wadada wanaolewa wakiwa na umri mdogo sana, miaka 13 hadi 18 ni msichana mkubwa kwa makabila mengi. So point zingine zitumike issues za moral/culture decay zinapoongelewa. Africa kama moja haina tamaduni/culture identity, tupo so different from one another. Unachokuabaliana nacho wewe kabila jingine litapinga. Mavazi ni tofauti sana, ila kitu kimoja in common ni kwamba yanaonesha sehemu kubwa ya mwili!

MPO!

Am watching!!

1 comment:

Anonymous said...

hi