Vijana wa Tanzania tunauwezo wa kufanya mabadiliko makubwa katika nchi hii kuliko kizazi kingine chochote kilichowahi kutokea since the Uhuru. Nasema hivi kwa sababu ni ukweli usiopingika ya kuwa kizazi chetu ndiyo kizazi kilichoelimika kwa wingi kulinganisha na vingine vyote vilivyopita. Asilimia kubwa ya vijana wa sasa wengi wamefika elimu ya secondary na kuendelea. Tumenufaika na globalization na kuwa kizazi kilichokuwa exposed to the outside world kuliko kizazi kingine chochote kilichopia. Vijana wa sasa tunaweza pata habari kirahisi kupitia simu za mkononi, television, internet, magazeti na vyanzo vingine vya habari.
Miaka 7 hadi 10 iliyopita lilikuwa jambo la ajabu kumkuta kijana wa miaka 14 hadi 18 akiwa na simu{ si simu ya tochi tuu bali advanced na zenye access to the internet}, lakini sasa hivi ni kitu cha kawaida tu.
Maendeleo haya yametuhakikishia kupevuka haraka kiakili na kuwa na mtazamo mpana sana, kuelimika mara nyingi kunamjenga mtu kutokukubali kuonewa, mfano tunaona migomo mingi vyuoni compare na miaka ya mababa na mamama zetu. Hii yote ni kutokana na kujifunza kutoka madarasani na dunia inayotuzunguka, kupitia globalization inasaidia kutupa ujasiri wa kusimamia haki.
Sasa tunatambua ya kuwa maendeleo ya mtu si kuwa na ‘uhuru na amani’ tuu, kwa hiyo campaign hizo hatuzitaki this year. Vijana wa the 21st Century tunatambua ‘uhuru na amani’ zinatakiwa zituletee social na economic development too. Miaka ya nyuma wanasiasa wengi wamewadanganya sana watu kutokana na kutoelemika kwao, JE VIJANA WA SASA TUTAKUBALI KUDANGANYWA PIA? Hell NO!
Kura zetu mkononi lets walk tall, tushiriki katika kupiga kura this year. ‘Giving up is not to wake up when you fall’ kwa hiyo usiwe na mentality yoyote mbovu ya kukuzuia kupiga kura. Maneno kama ‘hata ukimchagua Fulani, Yule mwingine atashinda tuu’ usiyape nafasi. Still believe in your vote na twende wote tukapige kura.
Tuachane na mentality ya kuwa siasa ni ya wazee na maneno mengine kama hayo, kumbuka viongozi watakaoingia madarakani effects za maamuzi yao hazitawa’affect wazee tuu. Kwa asilimia kubwa yatatu’affect sisi na our future lives.
Lets make this year’s election ZAMU YA KIJANA! VIJANA TUJITOKEZE KATIKA VOTING! THE LAST DROP CAN HAVE A HUGE EFFECT!!!!
Am watching!
![]()
2 comments:
Nakushukuru kaka yangu, maneno yako yamenijaza moyo wangu. Namshukuru Mungu kwa kunipatia vijana kama wewe. Endelea kutangaza mawazo yakO!
Ubovu nu kwamba kila mtu anataka kuwa kibali kama wazze wetu wakubwa.
Post a Comment