![]() |
| Wabunge Wa CHADEMA Walioshambuliwa! |
Hilo ndo swali ambalo limekuwa linakuja kwa akili yangu kwa sasa, kutoka Tunisia, Misri, Syria, na sehemu zingine, hivi demokrasia haikui bila vurugu na hata umwagaji wa damu? By-election za Arumeru zimepita na chaguzi za udiwani pia, tumeona yaliyotekea. Hii ni pamoja na kushambuliwa kwa wabunge wa chama cha Chadema..
Kitu muhimu cha kujua kwa sasa ni kwamba demokrasia inakuwa Tanzania, demokrasia ya matendo na si ile ya wimbo isiyoonekana kwa vitendo. Tunaona sasa watu wameamka na kufanya mabadiliko kidemokrasia lakini kwa wakati huo huo vurugu na mashambulio kwa watu mbalimbali wakati wa chaguzi na hata makongamano inaongezeka.
Hali ya ulinzi pindi za chaguzi na hata shughuli zingine za kisiasa miaka kumi na zaidi nyuma ilikuwa nyepesi na sio ya kutisha kwa maana ya jeshi kubwa la polisi kusimamia kama siku hizi. Na haya yote yanakuwa kwa wakati mmoja, wakati huo huo tunaona vurugu zinaongezeka na pia tunaona demkrasia ikizidi kujiidhihirisha na hapa ndo napojiuliza je ni kweli ukuaji wa demkrasia unaenda sambasamba na kukua kwa 'violence' (vurugu/vujo) katika jamii? Au hii inatokana na nguvu ya nyuma ya pazia na wale walio kwenye madaraka kuzuia kutolewa kwa kutaka kuwakatisha tamaa wale wanaowa'challenge au kujenga fikra mbovu na ya hofu kwa wapiga kura juu ya wapinzani?-hapa namaanisha kuwahusisha wapinzani na masuala fujo na vurugu.
![]() |
| Vijana Wamekuwa Kundi Kubwa na Muhimu Kwenye Kampeni Zote |
Naamini demokrasia ya kweli na yenye ukweli hata kwenye matokeo ya chaguzi katika bara la Afrika asa kwa nchi za chini ya jangwa la Sahara kama Tanzania inakuwa na inaweza kuwa ya kudhihirishwa kwa amani na haki.
Lakini kama kweli tunataka amani na usalama katika chaguzi na masuala yote ya kisiasa hatuna budi kutoa elimu zaidi kwa vijana. Naamini vurugu nyingi zinazotokea katika Tanzania na hata nchi zingine za Afrika nyakati za chaguzi na shughuli zingine za kisiasa kwa namna kubwa vijana ndo wanahusika, kuhusika kwao ni kwa kimatendo zaidi lakini kiuhalisia ni kuwa vijana tunatumiwa na wanasiasa wengine kwa manufaa yao.
![]() | |
| Wanasiasa Wameshatambua Umuhimu wa Vijana |
Juhudi zozote za kuleta amani na ukuaji wa demokrasia Tanzania na hata nchi zingine za Afrika lazima zifanyike pamoja na kuhusisha vijana watambue nafasi waliyonayo katika kujenga demokrasia kwa amani. Vijana wanatakiwa kupewa elimu ya demokrasia na elimu ya kutambua matokeo ya matendo na maamuzi yao katika mtakabali wa Taifa letu, bila kufanya hivi tunaweza kuliingiza taifa katika hali mbaya kutokana na kutumiwa huku vibaya na wanasiasa!
![]()



No comments:
Post a Comment