Tuesday, March 13, 2012

Kushindwa Kwa Nchi za Magharibi Kuchochea Mabadiliko Urusi; Nini Kinafuata?

Vladimir Putin.
Kwa watu wote wanaochukia tabia ya nchi za magharibi za kulazimisha mabadiliko katika nchi za wengine hasa zinazokuwa katika kiuchumi na nguvu za kidiplomasia watakuwa wamefurahishwa na kilichotokea Urusi, kwani juhudi zao hazikuzaa matunda.






Kweli Putin anakubalika na wengi wa wananchi wa Urusi, lakini tokea pilikapilika za uchaguzi zianze nchi hizi kwa kutumia mashirika mbalimbali ya kijamii yalianza kupiga kampeni za kumchafua Putin, hii ni pamoja na kukosoa kamati ya uchaguzi ya Urusi.





Hakuna ubishi ya kuwa hapa nia kuu ilikuwa kujaribu kutengeneza kitu kama walichofanya kule Libya, kutumia kundi dogo[minority] la wananchi wote kuchochea mabadiliko ya uongozi maarufu kwa lugha ya kingereza kama 'regime change'. Kinachotokea kwa sasa ni kwamba nchi hizi za magharibi zishatambua kuwa upande wao utakosa nguvu katika masuala ya kimataifa kwa kuwa nchi nyingi zinakua kwa kasi kiuchumi na nguvu za kidiplomasia nje ya familia ya NATO na washirika wengine wa nchi za magharibi. Hivyo njia pekee ya kuzuia hilo ni pamoja na kuchochea mabadiliko ya utawala na kuingiza serikali zitakazokuwa washirika kama ilivyotokea Libya, na hichi ndicho walichokuwa wanataka kitokee Urusi.

Hofu ya nchi nyingi kuwa na nguvu na kuungana na familia ya Uchina ni jambo ambalo mataifa ya magharibi hayatakuwa tayari kushuhudia. Kwa sababu hii ndio maana hata taifa la Irani linapata shida leo, hakuna ubishi ya kwamba kama Irani ingekuwa mshirika wa mataifa ya Magharibi lisingepata shinda yeyote kumiliki silaha za kinyuklia.

Ni ukweli usio na kificho ya kwamba tunapoelekea tutaona migogoro mingi zaidi kati ya nchi zinazokua kwa kasi kiuchumi na Marekani na washirika wake, ila hii itajitokeza hapo tu taifa usika alitakuwa tayari kupelekwa pelekwa na nchi za magharibi.

Kitakachofuata kwa Urusi chini ya Putin si jambo la kuficha mahisiano kati ya taifa la Urusi na nchi za magharibi yatakuwa magumu kidplomasia. Putin ashaonesha nia na kutangaza kuboresha zaidi mahusiano na taifa la Uchina kuliko Marekani na washirika wake, alitamka ya kuwa ni muhimu Uchina kwa kuwa wanaiheshimu Urusi na mambo yake ya ndani wakati nchi za magharibi haziheshimu taifa la Urusi.

Kwa wote tunaopenda amani na kuheshimu uhuru wa watu kuamua mabadiliko na kujiamulia viongozi wa mataifa yao bila kusukumwa kwa ubabe na nchi nyingine yeyote, wapenda uhuru wa kweli, tunawapongeza watu wa Urusi kwa kujiamulia mustakabali wa taifa lao bila kusikiliza propaganda za maadui wao.

No comments: